Wewe ni mwanachama? Ingia
Habari, karibu Kanono Group
Sisi watu wenye asili ya Wilaya za Karagwe na Kyerwa tunaoishi Arusha kwa pamoja, tumeamua kuanzisha umoja wetu ujulikanao kama KANONO GROUP ambao utaongozwa kwa mujibu wa Katiba hii kama nguzo na dira yake. Madhumuni ya Umoja yatakuwa ni yale tu yaliyoorodheshwa kwenye ibara ya tatu ya Katiba hii ambayo yanalenga kusaidiana na kushirikiana katika masuala ya elimu, na kuisaidia jamii nzima ya Watanzania hasa wale waishio katika mazingira magumu pale mfuko wa Umoja utakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Sifa za Mwanaumoja wa KANONO GROUP zitakuwa ni zile zilizoorodheshwa katika ibara ya nne ya Katiba hii. Umoja huu ulioanzishwa mwaka 1996 ulikuwa na Katiba. Kwa hiyo masuala yote yaliyomo katika katiba hii ni maboresho ya katiba zilizotangulia. Hadi sasa umoja una jumla ya familia zinazotambulika kama Wanaumoja 152 na vile vile Umoja unamilki mali. Kwa misingi hiyo Katiba hii inarithi madeni ya kudai na kudaiwa na mali zote za umoja zilizopatikana kipindi chote kabla ya kupitishwa na kutumika kwa Katiba hii.
Kumpatia Mwanaumoja ambaye atapata au mtegemezi wake atapata ubarikio, kipaimara au tukio jingine la kiimani lililokubaliwa na kutambuliwa kwa misingi ya imani ya dini yake.Huduma hii itatolewa kwa tukio moja kwa kila mwanaumoja au mtegemezi wake
Mwanaumoja atakayeolewa au kuoa atalipwa kiasi cha fedha kilichoainishwa kwenye kanuni za umoja. Mwanaumoja atakayefanya harusi ya kuoza binti au kijana kuoa atalipwa kiasi cha fedha kilichoainishwa kwenye kanuni za umoja.
Kumpatia mwanaumoja kiasi cha fedha kitakachoainishwa kwenye Kanuni kwa ajili ya nauli kwa msiba uliotokea sehemu ya mbali ambao kwa sababu za umbali wanaumoja wameshindwa kushiriki. Hii ni kwa wanaumoja ambao undugu wao na aliyefariki unatambuliwa na katiba.
Kumpatia mchango wa matibabu kwa mwanaumoja au mtegemezi mgonjwa ambaye amelazwa hospitali kwa siku tatu au zaidi. Huduma ya kulazwa hospitali inaweza kutolewa kwa mwanaumoja au mtegemzi mgonjwa ambaye kwa hali ya ugonjwa wake...